Mwongozo Wa Nguu Za Jadi

Mwongozo Wa Nguu Za Jadi

Schemes of Work,Lesson Plans,Primary Notes,Secondary Notes and Exams,Primary Exams,KCSE Revision Exams

Jalada, Anwani na Muhtasari

Katika jalada la riwaya ya Nguu za Jadi, kuna vitu anuwai vinavyoonekana, na vinaweza kuwa na fasiri mbalimbali kwa wasomaji tofautitofauti. Vitu vilivyopo kwenye mchoro wa jalada hilo ni:

a) Picha ya mwanamume mzee anayemzungumzia mvulana. Kutokana na wanavyoonekana, ni wazi wamefunikwa kwa kiwango cha haja na giza. Hii inaweza kuchukuliwa kama ishara ya mtoto wa kiume ambaye ametanzwa na matatizo,  ambaye hajapewa hadhi anayostahili katika jamii, kama inavyoonekana baadaye kwenye riwaya yenyewe.

b) Mbele ya picha ya mwanamume anayemzungumzia mvulana kuna uwanja usiokuwa  na mimea, pengine kutokana na uharibifu wa mazingira, jambo ambalo pia linajitokeza ndani ya riwaya.

c) Mbele huko kuna miti ambayo imefunikwa na giza kiasi, ambayo inaweza kuchukuliwa kuwakilisha matumaini yaliyonyimwa nafasi ya kujitokeza vizuri.

d) Nyuma ya miti kuna mlima mkubwa ulio na vilele (nguu) ambavyo vina mwangaza  juu. Hii inaweza kuchukuliwa kuwa ishara ya matatizo (mlima) na suluhu  inayopendekezwa na mwandishi ya kukabiliana na nguu (vikwazo) za tangu jadi zinazotatiza maendeleo ya jamii.

e) Nyuma ya mlima kuna mwanga hafifu unaojitokeza. Mwanga huu unaweza kuchukuliwa kuwa kiwakilishi cha matumaini mapya kwamba jamii iliyokumbwa na matatizo mengi kwa muda mrefu hatimaye inapata mwanga, kama inavyofanyika kwenye riwaya Lonare anapochaguliwa kuwa mtemi, jambo linaloipa nchi ya Matuo  matumaini mapya ya mabadiliko chanya.

 

Ufaafu wa Anwani: Nguu za Jadi

 

Nguu ni vilele vya milima. Katika riwaya hii, neno hili limetumiwa kisitiari, kuwakilisha vikwazo au matatizo yanayokumba jamii inayozungumziwa. Kwa hivyo, Nguu za Jadi ni vikwazo ambavyo vimekuwepo kama desturi au kanuni za maisha, na ambavyo vinadumaza maendeleo ya jamii.

Mifano ya vikwazo hivyo kutoka katika riwaya ni:

✔ Mila ambazo zinawadunisha wanawake na kuwanyima uhuru wa kujiendeleza.  Mifumo ya uongozi mbaya inayosababisha ufisadi, ukabila, utabaka, ubinafsi, hali ya kutowajibika, ufujaji wa mali za umma, uharibifu wa mazingira, ukiukaji wa haki za watoto, ukatili na wizi wa mali ya umma.

✔ Mifumo wa ubabedume uliokolea taasubi ya kiume wenye kudhalilisha wanawake na watoto wa kike.

✔ Mila zinazomnyima mtoto wa kiume nafasi ya kujiendeleza. Mila hizi zimemtelekeza mtoto wa kiume kwa kutothamini elimu na maendeleo yake.

✔ Umaskini uliokithiri.

✔ Matumizi na ulanguzi wa dawa za kulevya.

✔ Changamoto za ndoa na ukahaba.

 

Riwaya ya Nguu za Jadi kwa Muhtasari

Riwaya inapoanza, mhusika mkuu, Mangwasha, yuko na wanawe wawili, Sayore na Kajewa,  katika kanisa fulani, ambapo wanajificha. Nje ya kanisa hilo, wapo watu wengine wa kabila la Waketwa, waliokimbilia usalama hapo baada ya makao yao katika eneo la Matango  kuchomwa.

 

Kuna fununu kwamba jamii ya Waketwa inafurushwa kutoka makwao kwa sababu kuna watu  fulani wanaotaka ardhi ya Matango kwa nguvu.

 

Mtemi Lesulia, kiongozi wa nchi, anachukia kabila la Waketwa kwani yeyeanatoka katika kabila la Wakule. Waketwa na Wakule Wana uhasarna wa tangu jadi. Lonare, ambaye ni kiongozi wa Waketwa, ana urnaarufu mkubwa nchini. Katika uchaguzi mkuu uliopita,  alitekwa nyara na kwa namna hiyo, Mtemi Lesulia aliishia kuchaguliwa bila kupingwa.

Mwongozo Wa Nguu Za Jadi

Mangwasha ni mwanamke mwenye bidii, na anafanya kazi ya uhasibu katika afisi ya Chifu  Mshabaha. Chifu huyu ni rafiki mkubwa wa Mtemi Lesulia, naye pia anawachukia Waketwa.  Hivyo, anapanza kuwadhulumu Waketwa, jambo ambalo Mangwasha analifahamu kutokana na kufanya kazi naye. Chifu Mshabaha pia ni rafikiye Sagilu, mzee anayetaka kumuoa Mangwasha licha ya kwamba anajua msichana huyu ana mchumba, Mrima, na wanapanga ndoa. Siku ya harusi ya Mangwasha na Mrima, Sagilu anamtuma kimada wake, Sihaba,  akiwa na bomu lililofungwa kama zawadi kwa maharusi. Kwa bahati nzuri, watu  wanamshuku na maafa aliyokusudia kufanya hayafanyiki. Sagilu anamnyemelea Mrima na kumzuga kwa kutumia pesa kiasi kwamba Mrima anaisahau familia yake, huku akimwachia Mangwasha jukumu la kuwalea wana wao wawili.

 

Nchi ya Matuo inakumbwa na matatizo mengi. Kuna matatizoya kiuchumi yanayosababishwa na uongozi mbaya na ufisadi uliokithiri. Mtemi Lesulia anaendeleza ubaguzi dhidi ya Waketwa na vijana wengi walio na elimu hawapati kazi za kujiendeleza kimaisha. Kwa mfano, uteuzi wa wagombea nafasi za uongozi ukiwa umekaribia, machifu  wanalazimishwa kuwahamisha Waketwa kutoka Matango ili viongozi wanaopendelewa na mtemi wasipate upinzani, na yeye Mtemi Lesulia asishindwe na mpinzani wake mkuu wa kisiasa, Lonare. Sihaba anatumwa kwenda kuhakikisha kwamba makazi ya Waketwa yameteketezwa,

 

Anawatumia vijana ambao wanatumia petroli kuchoma makazi hap. Lonare na wafuasi wake wamepeleka kesi mahakamani, na akiwa na wenziwe, kama vile Ngoswe, wanawashawishi watu kurudi katika mako yao ya zamani kule Matango ambako wanajenga mahema. Hata hivyo, siku ya tatu, vijikaratasi vinasambazwa kuwataka watu watoke kwenye ardhi hiyo  ambayo, inabainika, imetwaliwa na kupewa Nanzia, mkewe

 

Mtemi Lesulia, na rafikiye mtemi, Mbwashu. Hawa wanataka kujenga jengo la kibiashara katika ardhi hiyo ya Matango. Watu wanaokuja kuanza ujenzi wanafukuzwa na Waketwa walioamua kuitetea ardhi yao kwa vyovyote vile. Baada ya kuona kwamba mpango wao umetibuka, Mtemi Lesulia anamtumia Sagilu kumpa Mrima pesa nyingi pamoja na  ahadi kwamba atapewa kazi serikalini, ilimradi amfanyie Mtemi Lesulia kampeni na kuwaendea kinyume Waketwa.

 

Kipindi kifupi kabla ya uteuzi wa watakaopeperusha bendera za vyama mbalimbali, Sagilu  anatofautiana na mwanawe, Mashauri, baada ya mwanawe kugundua kwamba babake ana uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake, Cheiya. Mtemi Lesulia naye anakosana na mwanawe, Ngoswe, wakati anapanga njama ya kuvuruga zoezi la uteuzi ili kuwaharibia wapinzani wake nafasi za kuteuliwa. Ngoswe anaona kwamba hatua ya babake inaongozwa na ubinafsi wa kujitakia uongozi na kutojali kwamba baadhi ya watu huenda wakapoteza maisha yao katika vurugu anazopanga. Sagilu anashindwa katika uteuzi na inakuwa wazi kwamba Mtemi Lesulia atakuwa na upinzani mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao. Kwa ushawishi wake, Chifu Mshabaha anafutwa kazi na mtemi anaamua kumwondokea Sagilu  ambaye sasa anaandamwa na sheria kwa ufisadi alioendesha nchini. Awali, tunaona Mangwasha akipoteza kazi yake katika afisi ya Chifu Mshabaha kwa kujitokeza kama mpinzani wa serikali kwani anamfanyia Lonare kampeni, kando na kwamba mara zote,  hakumkubalia Sagilu ombi la kumtaka awe kimada wake. Sihaba anatiwa mbaroni kwa kuendesha biashara haramu ya ukahaba inayosababisha wasichana wengi kuharibika lakini anaachiliwa kutokana na ushawishi aliokuwa nao serikalini. Mikasa hii inawaathiri wahusika wengi vibaya.

 

 

Sagilu anapatwa na kichaa na mkewe mtemi, Nanzia, anaugua baada ya jengo lake la kibiashara la Skyline Mall kutwaliwa. Baada ya kulazwa hospitalini kwa muda, anafariki.

 

Kwa mara nyingine, Lonare anatekwa nyara kabla ya uchaguzi lakini anafaulu kutoroka na kupata matibabu. Uchaguzi mkuu unafanyika na Lonare anachaguliwa kuwa mtemi. Rafikiye Sagilu anashindwa na Mwamba anayechaguliwa kuwa mbunge wa Matango. Lonare anawahutubia wananchi wa Matuo na kuahidi kuufufua uchumi wa nchi na kukabiliana na ufisadi serikalini. Anaahidi pia kwamba serikali yake itashughulikia tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na kuhakikisha kwamba pana usawa wa kijinsia, akisema kwamba Matuo  imesambaratishwa na ubabedume. Anawaomba wananchi wenzake kujiepusha na ukabila na kuwahimiza kukataa na kufichua maovu yanapofanyika nchini. Lonare anachagua kutolipiza kisasi dhidi ya mahasidi wake wa kisiasa.

 

 

Sura ya Kwanza

 

Mangwasha yuko na wanawe katika kanisa fulani ambapo yeye na watu wa kabila lake la Waketwa wamekimbilia usalama baada ya kuchomewa nyumba zao katika mtaa wa Matango, jijini Taria. Kuna fununu zinazosema kwamba pana watu fulani waliotaka kuitwaa ardhi ya Matango kwa nguvu. Inabainika pia kwamba mjini Taria, kuna jamii mbili ambazo  ni mahasimu wa tangu jadi, Wakule na Waketwa. Mtemi Lesulia, kiongozi wa nchi, anatoka katika jamii ya Wakule na anawachukia Waketwa. Lonare ni kiongozi wa Waketwa lakini ana umaarufu mkubwa nchini kote kwani katika uchaguzi mkuu uliopita, alikuwa na sera bora zaidi. Hata hivyo, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi, alitekwa nyara na Mtemi Lesulia kuchaguliwa bila kupingwa. Mangwasha anafanya kazi ya uhasibu katika afisi ya Chifu  Mshabaha. Anajua kwamba Chifu Mshabaha, ambaye pia anawachukia Waketwa, anafanya mpango wa kuwadhulumu Waketwa. Kwa sababu hii, anapanga kumwona kiongozi wake,  Lonare, ili kumweleza njama zinazopangwa dhidi ya watu wake.

 

Juhudi za Mangwasha, hata hivyo, zinatatizwa na hali kwamba jamii haimthamini mwanamke, na anashangaa kama atasikilizwa. Anaamua atafanya tu alilokusudia, liwe liwalo.

Mwongozo Wa Nguu Za Jadi

Masuala makuu yanayojitokeza katika Sura ya Kwanza

 

✔ Uhasama wa kikabila na kisiasa unajitokeza kwani Waketwa wanabaguliwa na kupokwa haki zao za kumiliki ardhi na kuishi kwa amani. Waketwa wanalaumiwa hata kwa mambo ambayo hayako katika uwezo wa binadamu kudhibiti, kama vile maradhi sugu  yanapowashinda madaktari. Kiongozi wa Waketwa, Lonare ameepuka kifo mara nyingi,  kifo kilichopangwa na Wakule.

✔ Ukabila ulioshamiri Matuo unawafanya Waketwa wengi kuwa katika tabaka la chini,  huku wakiwa na viongozi wachache sana serikalini.

✔ Mfumo wa ubabedume unawanyima wanawake nafasi ya kujiamini kama wahusika sawa katika jamii. Mwanamke asiyekuwa na cheo au pesa hawezi kusikilizwa (uk. 8).  ✔ Ufisadi umeshamiri katika jamii. Ardhi ya Waketwa inapotwaliwa, Chifu Mshabaha anaangalia kando kwani ameshapokea mlungula (uk. 9).

✔ Maudhui ya bidii yanajitokeza kupitia kwa mhusika Mangwasha ambaye msimulizi anasema alifunzwa kuuambaa uvivu (uk. 12).

Mwongozo Wa Nguu Za Jadi

Download here if you are a member.

 

MWONGOZO WA CHOZI LA HERI(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA TUMBO LISHILOSHIBA NA HADIDITHI ZINGINE
MWONGOZO WA KIGOGO NOTES(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA CHOZI LA HERI NOTES(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA TUMBO LISHILOSHIBA(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA KIDAGAA KIMEMWOZEA(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA KIGOGO(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA KIGOGO NOTES(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
MWONGOZO WA CHECHE ZA MOTO
MWONGOZO WA TUMBO LISHILOSHIBA(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE(Opens in a new browser tab)
arise shine KCSE 2022 trials EXAMS MOCK(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA KIGOGO NOTES(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA MAPAMBAZUKO YA MACHWEO(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA CHOZI LA HERI NOTES(Opens in a new browser tab)
2022 MOI TEA MOCK ANSWERS(Opens in a new browser tab)
bembea ya maisha mwongozo(Opens in a new browser tab)
2022 SUNRISE EVALUATION EXAMS(Opens in a new browser tab)
2022 ASUMBI POST MOCK REVISION EXAMS