MWONGOZO WA MAPAMBAZUKO YA MACHWEO

MWONGOZO WA MAPAMBAZUKO YA MACHWEO

MWONGOZO WA MAPAMBAZUKO YA MACHWEO



If you need mwongozo wa mapambazuuko ya machweo
send sh180 , lipa na mpesa , buy goods — till no. 5169393

Then text 0722546300 ,We will send it in you email /whatsapp immediately.



Utangulizi
Mwongozo huu una nia ya kuwa mwanga gizani kwa wasomi wa diwani ya >Mapambazuko ya Machweo na
Hadithi nyingine, kwa kutoa maelezo maridhawa kuhusiana na hadithi tofauti zilizomo humu. Ili kufaniki sha
hili, mwongozo huu umeangazia masuala kadhaa katikahadithi. Kabla ya kwenda katika hadithi binafsi, ni
vyema kuangazia vipengele Fulani vya diwani.
Mada: Mapambazuko ya Machweo.
Mada ya diwani za hadithi fupi huwa ni mada ya mojawapo wa hadithi zilizomo. Hata hivyo, sharti iwe
mada ya kuvutia wasomaji na pia yenye kubeba uzito katika diwani husika. Lnafaa kuwa mada ambayo ina
uzito wa kutosha kubeba ujumbe wa diwani.
Mada >Mpambazuko ya Machweo?, ina athari ya kipekeekwa msomaji. Mapambazuko ni majira ya alfajiri,
kabla ya jua kuchomoza hali Machweo ni wakati wa jioni, jua linapotua. Ukinzani katika mada unazua
taharuki kwa msomaji, ambayo inamtuma kupitia hadit hi za diwani hiyo ili kufahamu vipi Mambazuko
yanatukia wakati wa Machweo.
Mada hii inaleta fikra tofauti. Kwanza, ujumbe wake unaweza kurejelea hali ya mafanikio baada ya tabu
tele. Isitoshe, majira haya yananweza kurejelea umri, mapambazuko yakirejelea ujana nayo machw eo uzee.
Inaweza pia kumaanisha mafanikio katika machweo ya maisha(uzee).
Mada hii, hivyo basi, inabeba taarifa muhimu kwa ajili ya diwani nzima. Suala la matumaini au mafaniki o
katika/baada ya taabu limesawiriwa katika hadithi nyingi kwenye diwani hii. Hivyo, tunaweza kusema mada
hii imefumbata ujumbe wa diwani nzima. Mifani ya hadithi zinazodhihirisha hali ya >Mapambazuko ya
Machweo? ni kama?Mapambazuko ya Machweo?, >Fadhila za Punda?, >Toba ya Kalia?, >Nipe Nafasi?,
>Ahadi ni Deni?, >Sabina? na nyinginez o.
Hivyo basi, ni wazi kwamba mada >Mapambazuko ya Machweo? inafaa kabisa kwa diwani hii.
Jalada:
Jalada katika diwani ya hadithi fupi aghalabu hubeba ujumbe wa hadithi iliyobeba anwani. Hali si tofauti
katika diwani hii. Jalada linaakisi hali katika hadit hi ya >Mapambazuko ya Machweo.
Kuna bwana aliyevaa suti ambaye anaingia kwenye gari. Haikosi huyo ni Makutwa, anayemiliki gari la
kibinafsi pekee mjini Kazakamba.
Kando yake, kuna mwanamume na mwanamke wanaoonekana kuwa katika hali ya majibizano kwa jinsi
walivyoinua mikono, mwanamume mkono wa kulia na mwnamke mkono wa kushoto nyuso zikielekeana.
Hawa bila shaka ni Makucha na mkewe Macheo ambao wana mjadala mara kwa mara kuhusiana na suala la
Makutwa kumkebehi Makucha.
Kando ya wawili hao pembeni kulia, kuna kimeza kidogo chenye vifaa fulani na kiti chake. Haikosi hapo ni
sehemu anapouzia vitafunio Makucha. Pembeni kulia kulia nako kuna sehemu ya nyumba, ambayo itakuwa
ya Makucha na mkewe Macheo.
Mbele yao mbali kidogo, kuna watoto wadogo wanaoonekana kuwa k atika shughuli za kuzoa mchanga.
Hawa ni watoto ambao Makutwa anawatumikisha katika mgodi wake kinyume cha sheria.

 


In Kiswahili, Cheche za Moto by John Habwe (Jomo Kenyatta Foundation) will be studied as the compulsory novel, replacing Chozi La Heri by Assumpta K Matei (One Planet Publishers).


Mapambazuko ya Machweo (Mountain Top Publishers) will be the new anthology of short stories, replacing Tumbo Lisiloshiba (Longhorn Publishers).



MWONGOZO WA CHOZI LA HERI(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA TUMBO LISHILOSHIBA NA HADIDITHI ZINGINE
MWONGOZO WA KIGOGO NOTES(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA CHOZI LA HERI NOTES(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA TUMBO LISHILOSHIBA(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA KIDAGAA KIMEMWOZEA(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA KIGOGO(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA KIGOGO NOTES(Opens in a new browser tab)
MWONGOZO WA TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
MWONGOZO WA CHECHE ZA MOTO