MWONGOZO WA CHOZI LA HERI

MWONGOZO WA CHOZI LA HERI

MWONGOZO WA CHOZI LA HERI


Click here to download whole MWONGOZO WA CHOZI LA HERI

JALADA


Jalada la Riwaya ya Chozi la Heri ni tokeo la usanii  wake , Robert Kambo. Katika upande wa mbele  sehemu ya juu, mna rangi ya kijani kibichi iliyokolea.
Maana ya rangi hii ni uhai na rutuba. Riwayani yamo maeneo yaliyo na rutuba yanayotoa mazao mengi.

Katika eneo la Msitu wa Heri alikoishi Ridhaa kwa  miongo mitano, mwanzoni kulikuwa kama jangwa la Kalahari lakini Ridhaa alihakikisha kuwa kijiji hiki
kimepata maji ya mabomba hadi eneo zima likatwaa  rangi ya chanikiwiti. Miti mingi kama Miambakofi, mivule na miti mingine kapandwa. Maeneo mengme yaliyokuwa na rutuba ni kama Msitu wa Mamba.

Watu waliogura makwao  walipohamia hapa walikata miti na kupanda vyakula  kama mahindi ambayo yalifanya vizuri mno. Ndam ya rangi hii mna anwani ya kazi iliyoandikwa  kwa rangi nyeupe. Kawaida rangi hii huashiria amani. Licha ya mambo kuwaendea vibaya wahusika wengi riwayani, hatimaye mna amani ya kudumu.

Jina lake mwandishi liko maeneo yayo hayo na  limeandikwa kwa rangi ya manjano. Rangi hii huashira ukomavu. Mwandishi wa riwaya hii ni mwenye tajriba pana. Amekomaa katika uandishi wa kazi za fasihi. Masuala anayoyaangazia ni yale
yanayoiathiri jamii yake. Ametumia mtindo unaoashiria upeo wa ukomavu wake.

Upande wa chini wa jalada la riwaya hii mna mchoro wa jicho. Jicho hili linadondokwa na chozi. Ndani ya chozi mna watu watatu(mmoja wa kike na wawili wa
kiume). Inahalisi kuwa watu hawa watatu ni Umu, Dick na Mwaliko. Walifurahl mno walipokutana wote  katika hoteli ya Majaliwa. Riwayani, Umu na Dick  walikimbia wote kwa pamoja na wakamkumbatia  ndugu yao Mwaliko na huku wakaanza kulia na  kutokwa na machozi ya faraja heri.

Click here to download whole MWONGOZO WA CHOZI LA HERI